Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akizungumza jambo kabla ya uzinduzi huo.
…Akifafanua jambo.
Baadhi ya wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo, akiwemo msanii nguli wa mashairi, Mrisho Mpoto (wa pili kushoto).
Baadhi ya akina mamalishe waliohudhuria hafla hiyo.
Wadau mbalimbali wakifuatilia uzinduzi uliokuwa ukiendelea.

.Mwalimu akikata utepe kama ishara ya uzinduzi huo.

…Akiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Basilla Mwanukuzi akizungumza jambo.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, leo amezindua rasmi taasisi ya Basilla Mwanukuzi inayojishughulisha na kutoa elimu, mikopo kwa akina mamalishe.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Saalm, mkurugenzi wa taasisi hiyo ambaye pia ni Miss Tanzania 1998, Basilla Mwanukuzi, alisema lengo ni kuwawezesha wanawake kuinua uwezo wa kiubunifu na kiuchumi na kuwasaidia wanawake wa makundi tofauti kujitoa kutoka kwenye hali ya kusaidiwa hadi kuweza kusimamia miradi yao wenyewe na hivyo kubadili hali zao maisha.
Alisema sehemu ya uzinduzi wa mradi huo pia itawawezesha kupata elimu ya ujasiriamali, afya pamoja na kupika chakula bora chenye kuzingatia virutubisho na uwezeshaji wa kupata mikopo na kuongeza mitaji yao.
“Taasisi yangu iliguswa na changamoto nyingi wanazokabiliana nazo mamalishe kwa kipindi kirefu bila msaada wowote baada ya kufanya utafiti kwa muda na kuzungumza na mamalishe nikagundua changamoto zao ikiwemo ukosefu wa mitaji, hivyo mradi huu utawasaidia watambulike, waweze kujiamini na kupewa thamani katika jamii,” alisema Mwanukuzi.
Alisema utekelezaji wa mradi wa Wezesha Mamalishe pia utajumuisha uundaji wa vikundi vya ushirikiano ili kubadilishana uzoefu na uanzishaji wa shughuli za kujiingizia kipato kama utafutaji wa tenda za kuandaa vyakula vya harusi na kadhalika.
Alifafanua kuwa hadi sasa mradi huo umefanikiwa kuwaandikisha mamalishe waliopo jijini Dar es Salaam, na baadhi yao wameanza kupata mikopo ya riba ndogo kupitia benki ya Covenant, huku wakiendelea kupanua wigo kufikia nchi nzima.
Naye Waziziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alimpongeza Mwanukuzi kwa kuanzisha taasisi hiyo kwani itawasaidia kuwainua mamalishe kutoka hali ya chini na kuwa hali nzuri hivyo akasisitiza kuwa serikali inatambua mchango unaotolewa na taasisi mbalimbali huku akiahidi kutoa ushirikiano ili kuwakwamua wanawake wajasiriamali.
Na Denis Mtima/Gpl