Kutoka kushoto ni Mratibu wa maandalizi ya mkutano huo, Margareth Bwathondi, Mkuu wa Wilaya ya Rorya,Felix J.Lyaniva na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Damian George.
Mkuu huyo akitoa ufafanuzi wa jambo kwa wanahabari baada ya kuulizwa maswali. Hawapo pichani.
MKUU wa Wilaya ya rorya Mkoani Mara anatarajia kufanya mkutano wake na wanarorya waishio jijini Dar es Salaam Jumapili saa nane mchana Aprili 17 mwaka huu katika ukumbi wa Karimjee Dar.
Hayo ameyasema leo Mkuu huyo, Felix J. Lyaniva alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar ambapo amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuwakaribisha wanarorya waishio jijini Dar es Salaam pamoja na wa maeneo mengine kwenda katika wilaya hiyo kwa ajili ya kuwekeza katika fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya wilaya hiyo.
Amesema katika kuwaeleza fursa hizo zilizopo ndani ya wilaya yake pia atawaeleza baadhi ya changamoto ambazo pia wanaweza kuzizungumzuia ili kuweza kuzipatia ufumbuzi .
Alifafamua kuwa wilaya yake kutokana na kuwepo kandokando ya ziwa Victoria inazofursa nyingi za uwekezaji kwenye nyanja kama vile za gesi asilia ya Helium, dhahabu, uvuvi, utalii, kilimo, mifugo na usafirishaji hasa ukizingatia inapakana na nchi za jirani za Kenya na Uganda na kupelekea kuwa mahala pazuri kwa biashara ndani na nje ya nchi.
Lyaniva aliwataka wadau mbalimbali wa maendeleo, pamoja na wanarory waishio Dar na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi ambapo pia viongozi wa ngazi za juu wa wilaya hiyo nao pia watakuwepo kushiriki mkutano huo.
NA DENIS MTIMA/GPL