ILIPOISHIA RISASI JUMATANO:
“Rehema amenitukana sana, hivi hapa afadhali niondoke kwenye nyumba hii,” nilisema nikichukua kanga na kuivaa…
“Yuko wapi?”
“Sebuleni…”
Baba Rehema alitoka kitandani, akaninyang’anya kanga, akajifunga na kutoka. Mimi nilitoka na taulo lake ili nikasikilize…
KIMBIA NAYO MWENYEWE…
“We Rehema,” alimuita mwanaye huku akiwa anakaa kwenye kochi…
“Abee baba…shikamoo baba…”
“Achana na shikamoo yako…kwa nini umemtukana Jamila?”
“Nimemtukanaje baba?”
“We si umemtukana,” alisema tena baba Rehema.
Rehema alisema hajanitukana na mimi nikakazia kwamba alinitukana. Baba Rehema akaniuliza alinitukanaje? Nikashindwa cha kusema na kubaki natunga tusi kichwani na kumwambia baba Rehema…
“Hapana Jamila…hapana…Rehema ni mwanangu, namjua. Hawezi kutukana tusi kama hilo,” baba Rehema alinishushua nikashushuka mwenyewe…
“Sasa sikia Rehema…kuanzia leo huyu Jamila muite mama… unasikia?”
Rehema alikataa kwa kutingisha kichwa juu chini…
“Una maanisha nini kutingisha kichwa?” baba Rehema alimuuliza mwanaye…
“Mimi simtaki Jamila awe mama yangu,” alisema Rehema bila woga.
Mimi nilihisi kwamba, Rehema ndiye atakayekuwa kikwazo cha mimi na umama wa nyumba…
“Kama ananikataa na udogo huu je, baba yake akifa na yeye ameshapata akili si ataniua?” nilijiuliza mwenyewe ikabidi nikazane kumuweka sawa baba yake…
“Mpenzi huyu ni mtoto wetu sote, ongea naye polepole atakuelewa tu. Usimlazimishe. Rehema ni mtoto mzuri sana, ana adabu, heshima,” nilisema…
“Eti Rehema…Jamila ni mama yako si ndiyo mwanangu?”
Rehema alinyamaza kimya huku akiniangalia mimi na kumwangalia baba yake kwa zamu…
“Rehema…”
“Abee…”
“Huyu nani?”
“Dada Jamila…”
“Ambaye sasa ni nani mwanangu?”
“Mama…”
“Ee mama…kuanzia leo Rehema ni nani?”
“Ni mama…”
“Safi sana mwanangu mzuri, njoo nikukumbatie basi,” alisema baba Rehema na kumshika mwanaye, akamfuata na akambusu…
“Mmmwaa…”
Nilitumia nafasi hiyo kumwita Rehema maana mimi nilikuwa nimekaa kwenye kochi kubwa…
“Njoo mwanangu Rehema.”
Rehema alinifuata na kukaa kwenye mapaja yangu, nikambusu na kumkumbatia kwa upendo wote…
“Mimi nani?” nilimuuliza…
“Wewe mama.”
“Safi sana.”
Nilisimama na Rehema na kwenda naye jikoni ambako nilimuandalia chakula, tukarudi hadi sebuleni na kumuwekea ale!
“Kula chakula mwanangu ee!”
“Asante mama,” Rehema aliniita mama mpaka raha.
Muda huo, baba Rehema alikuwa amerudi chumbani baada ya kuweka sawa hali ya hewa ya kichwani kwa Rehema. Hivyo wakati Rehema anakula na mimi nikaenda chumbani…
“Nimefurahi sana mume wangu kukubalika na Rehema ndiye aliyekuwa ananipa wakati mgumu,” nilimwambia baba yake…
“Wewe wasiwasi wako tu, mtoto kama yule hawezi kukushindwa hata siku moja…”
“Kweli lakini mpenzi wangu maneno yako nakubaliana na wewe,” nilisema huku nikimwonesha waziwazi kwamba nataka mechi.
Na yeye bila hiyana wala kinyongo alinipa ushirikiano wa kutosha. Alinigeukia na kunivutia kwake, nikasogea, akaniletea ulimi ukiwa tayari kwa kuomba njia kinywani mwangu.
Sijui kwa sababu ya furaha, siku hiyo nilijikuta nataka mechi haraka sana hata kama refa alikuwa hajaingia uwanjani…
“Mpenzi mume wangu,” nilimuita baba Rehema…
“Niambie mke wangu Jamila.”
Nilimtazama baba Rehema kisha nikashusha pumzi kwa nguvu na kumuweka sawasawa kwa mchezo unaofuata…
“Baba…baba…babaa,” sauti ya Rehema iliita kutokea sebuleni kuja chumbani…
Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi Jumatano ijayo.
SOCIAL MEDIA ZETU:
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz