×

Droo ya Jishindie na DSTV Kampeni yafanyika leo

1

 Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (kushoto) akichezesha droo hiyo huku meneja masoko wa kampuni hiyo, Furaha Samalu na meneja uhifadhi, Hilda Nakajumo wakishuhudia.

2

Meneja Uhifadhi wa DSTV, Hilda Nakajumo (wa pili kulia) akizungumza kwa simu na mmoja wa washindi wa droo hiyo.

3Wafanyakazi wa DSTV wakiwa pamoja na Mkaguzi Mwandamizi wa Kampuni ya Garming Board of Tanzania, Mrisho Milao (kulia), wakati droo hiyo ikichezeshwa.

LEO Jumanne, Kampuni ya Multichoice Tanzania kupitia huduma zake za DSTV, ilichezesha droo ya Jishindie na DSTV Kampeni ambapo wateja wake zaidi ya 100 walijinyakulia zawadi mbalimbali.

Katika droo hiyo iliyoshuhudiwa na Mkaguzi Mwandamizi wa Kampuni ya Garming Board of Tanzania, Mrisho Milao, iligawanywa katika vipengele vitatu.

Droo ya kwanza ambayo ilikuwa ikiwahusisha wateja wapya wa DSTV waliojiunga kuanzia Januari, mwaka huu na kuitumia huduma hiyo kwa miezi mitatu mfululizo bila ya kukatika, iliwapata washindi wawili ambao ni Mwelly Nyakusaima wa Igoma, Mwanza na Evarist Ndambo wa Tabata, Dar. Washindi hao watapelekwa Zanzibar pamoja na familia zao na kukaa huko kwa siku mbili.

Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu, amesema: “Droo ya pili iliwashirikisha wateja wetu wa zamani wote ambao wamekuwa ‘active’ kwa mwaka mmoja, na hapa tumewapata washindi 50 na kila mmoja tutampatia king’amuzi cha DSTV Explora.

“Pia washindi wengine 90 wa droo ya tatu ambao hawa ni wale waliotimiza mwaka mmoja, wao tutawapatia vifurushi mbalimbali vya mwezi kutoka DSTV.”

Picha/ Stori na Omary Mdose/GPL

Leave a Comment