×

Mkude: Tusipopanda ndege, nasepa Simba

mkude

Kiungo wa Simba, Jonas Mkude.

Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam
HEH yamekuwa hayo! Kwani kiungo wa Simba, Jonas Mkude, amesema kama timu yake isipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ataondoka klabuni hapo ili akachezee timu nyingine msimu ujao.

Mkude ameliambia Championi Jumatano kuwa, ndoto yake kubwa ni kushiriki michuano ya kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ngazi ya klabu na si vinginevyo.

Nafasi pekee ya Simba kushiriki michuano hiyo ambayo ni Ligi ya Mabingwa Afrika au Kombe la Shirikisho Afrika, ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwani tayari imetolewa kwenye Kombe la FA.

KUSOMA HABARI HII KWA KINA ZAIDI, JIPATIE NAKALA YAKO YA CHAMPIONI JUMATANO, APRIL 20, 2014

 

Leave a Comment