Na Nathaniel Limu, AMANI
SINGIDA: Ukatili! Kijana
mmoja mwenye umri wa
miaka 32 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida
Mjini kwa madai ya kumbaka mara tatu kikongwe mwenye umri wa miaka 84, mkazi wa Kijiji cha Chungu wilayani Ikungi wiki iliyopita. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka
bibi huyo ambaye jina lake linahifadhiwa, alifanyiwa kitendo hicho mara mbili, kabla ya mtego
kuwekwa uliomnasa kijana huyo wakati alipokwenda kumfanyia ukatili huo kwa mara ya tatu.Baada ya kutajwa na kuahirishwa kwa shauri hilo, duru za kimahakama zinasema kesi
hiyo katika kikao chake kijacho, itaanza kusikiliza ushahidi kutoka upande wa mashtaka. Katika viwanja vya mahakama, majirani wa bibi kizee huyo walionekana kumbeba ili kumpeleka kwenye gari, kwani alishindwa kutembea mwenyewe pasipo kupewa msaada kutokana na umri wake
mkubwa. Kijana anayetuhumiwa kufanya kitendo hicho cha kinyama alirudishwa mahabusu kusubiri siku ya kesi hiyo iliyopangwa kuanza kusikilizwa mapema wiki ijayo.