×

Dogo Janja, …mchezo huu hauhitaji hasira

philipPhilip Boardman ‘Admiral P’

Mwaka 1982 katika Jiji la Lusaka, Zambia alizaliwa Philip Boardman ‘Admiral P’ ambaye alikuja kuwa na uraia wa nchi mbili ambapo baba yake alikuwa ni Mnorway na mama Mzambia.

Miaka 13 baadaye baba wa Admiral, Tom Boardman akiwa nchini Zambia aliugua sana na kulazimika kwenda kutibiwa katika Jiji la Oslo, Norway na hapo ndipo ukawa mwanzo wa Admiral kuishi nchini Norway.

Sasa hivi, Admiral ni bonge moja la mwanamuziki wa Reggae nchini Norway akiwa na albamu tatu hadi sasa ambapo 2008 alitoa albamu yake ya kwanza ya Muzikal Bullit, ya pili 2009 iitwayo To The World na ya mwisho aliitoa mwaka 2014 iitwayo Selvitillit & Tro.

Katika Albamu ya Selvitillit & Tro kulikuwa na wimbo mmoja uitwao Hatere akishirikiana na rapa kutoka nchini humo, Onkl P uliotokea kuteka sana mashabiki wa Reggae hususan nchini Norway kwa jinsi alivyoimba na mdundo wake ulivyo.
Miezi michache iliyopita, prodyuza kutoka Norway, Carl Hovind alitua Bongo na lengo kubwa ni kufanya kazi na wasanii Wabongo kuleta ladha tofauti na moja ya ngoma aliyopika ni pamoja na My Life ya Dogo Janja.

fab5dogo2Bjanja2Bmy2BlifeDogo Janja

My Life imekuwa miongoni mwa ngoma zinazopendwa zaidi Bongo kutokana na mdundo na alivyoimba Dogo Janja.
Kupitia ngoma hiyo imemrudisha tena Dogo Janja aliyeonekana kama ameanza kupotea kwenye gemu.

Lakini sasa kama ukisikiliza kwa makini Ngoma ya Hatere ya Admiral kisha ukasikiliza My Life ya Dogo Janja ni wazi utaelewa nachomaanisha. (kukopi na kupesti)

Kwa mujibu wa Dogo Janja, awali hakuwa akijua kama biti hiyo imeshatumika lakini baada ya ngoma kutoka alikuja kutambua kuwa ilishawahi kutumika miaka ya nyuma na Admiral P.

880A1920-1Carl Hovind

Swali linakuja, aliyeanza kutumia mdundo na ‘melodi’ ni Admiral kutoka Norway, prodyuza aliyetengeneza Carl Hovind kutoka Norway, msanii aliyetengenezwa ambaye hakuwa anajua (Dogo Janja) anatoka Bongo.

Ina maana prodyuza hakuliweka wazi hili la kukopi na kupesti biti na sehemu ya melodi kwa msanii?
Hauhitaji digrii kuweza kulijibu swali kama hili jepesi, kifupi mchezo uliofanyika wala hauhitaji hasira!

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, DOWNLOAD NA INSTALL APP HII ILIYOPO KWENYE PLAY STORE YAKO==>VODACOM M-PAPER APP

*********

 

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave a Comment