×

Waya wa Umeme Ulioning’inia Barabarani Wazua Taharuki

1Magari yakipita huku waya wa umeme ukiwa umening’inia.3Hali ilivyokuwa huku madereva wakijitahidi kuukwepa waya huo.5Foleni kubwa huku magari yakilazimika kutumia njia moja badala ya njia mbili zilizopo upande mmoja wa barabara hiyo.

HATARI! Mchana wa leo katika eneo la Tabata-Gereji jijini Dar, kwenye barabara ya Mandela kumeonekana waya wa umeme ulioning’inia katikati ya barabarani hiyo huku hali hiyo ikisababisha foleni kubwa ya magari hivyo kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Hali hiyo imezua taflani kwa wakazi wa eneo hilo na watumiaji wa barabara hiyo kwani wamekuwa wakipita eneo hilo ambapo waya huo umening’inia na kufunga upande mmoja wa barabara hivyo madereva wamelazimika kutumia njia moja badala ya njia mbili zilizopo kwenye barabara hiyo.

Mmoja wa maderva hao alisema: “Tunawaomba Tanesco waje walishughulikie suala hili mapema, huu waya ulioning’inia umeasababisha foleni kubwa kwani umeziba njia moja hivyo tunalazimika kubanana kwenye njia hii nyingine.”

“Mbali na hivyo kuna hatari zaidi endapo mtu ataugusa waya huo bila kujua anaweza kupigwa short na kufa kabisa.” Alisema dereva huyo.

Tatizo kubwa zaidi litakuja endapo itafika usiku tatizo hili halijafanyiwa ufumbuzi, mtu atakuja usiku akiwa spidi anaendesha ataukwaa huu waya, atapigwa shoti ya umeme na kufa au kuumia vibaya hivyo mamlaka husika waliangalie hilo mapema,” alisema Mussa Shabani mkazi wa Tabata-Gereji.

WITO WETU: Wakazi wa Tabata-Gereji na watumiaji wa barabara ya Mandela mnaombwa msiuuguse huo waya kwani ni hatari, lakini pia TANESCO wanaombwa wafike eneo hilo ili kufanya marekebisho ya waya huo na wananchi waendelee kuitumia barabara hiyo kwa amani.

PICHA NA DENIS MTIMA/GPL

KUFAHAMU YOTE HAYA NA MENGINE, NUNUA GAZETI LA IJUMAA, LEO April 22, 2016

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave a Comment