×

Miss Dar City Centre 2016 kuzinduliwa Jumamosi hii

SHINDANO la kusaka warembo lijulikanalo kama Zan Aqua Miss Dar City Centre linatarajiwa kuzinduliwa rasmi Jumamosi hii, Aprili 23 ndani ya Ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar.

mratibu wa Zan Aqua Miss Dar City Centre 2016, Nancy Joseph akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).

Mratibu wa Zan Aqua Miss Dar City Centre 2016, Nancy Joseph akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).

Akizungumza na Global TV Online katika kikao na waandishi wa habari, Nancy Joseph ambaye ni mratibu wa shindano hilo alisema kuwa, ufunguzi huo ni maalum kwa ajili ya kuelekea katika shindano lenyewe litakalofanyika Mei 21, mwaka huu.

Afisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda akifafanua kitu ndani ya mkutano huo.

Afisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda akifafanua kitu ndani ya mkutano huo.

“Shindano la mwaka huu litakuwa likijulikana kama Zan Aqua Miss Dar City Centre ambapo litafanyika katika Hoteli ya Golden Tulip City Centre na waahidi tu mwaka huu tumejipanga zaidi na mtegemee kuwa shindano la kipekee kuliko yaliyotangulia,” alisema Nancy.

kutoka kushoto, mkuu wa masoko Golden Tulip City Centre, Catherine Kisaka, Afisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda pamoja na mratibu wa shindano hilo, Nancy Joseph.

Kutoka kushoto, mkuu wa masoko Golden Tulip City Centre, Catherine Kisaka, Afisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda pamoja na mratibu wa shindano hilo, Nancy Joseph.

Mara ya mwisho kufanyika shindano hili lilikuwa likitambulika kama Red’s Miss Dar City Centre ambapo ilikuwa mwaka 2014 na mrembo Jihan Dimechk aliibuka kidedea.

Nancy akisikiliza swali kutoka kwa mwandishi (hayupo pichani).

Nancy akisikiliza swali kutoka kwa mwandishi (hayupo pichani).

waandishi wakisikiliza mkutano huo.

Waandishi wakisikiliza mkutano huo.

Shindano hili limedhaminiwa na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers, Golden Tulip Dar City Centre, TV1, Zan Aqua (Maji ya kunywa), M&J Printing pamoja na Super Model Collections.

DSC_8251

Aliyekuwa Mshindi wa Miss Dar City Centre 2014, Jihan Dimechk (katikati).

 

Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

 

 

Leave a Comment