Kamera za tovuti hii leo zimenasa taswira saba za mabasi yaendayo kasi yakiwa katika majaribio kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabasi hayo ya Mradi wa Dart yanatarajia kuanza rasmi kutoa huduma Mei 10, mwaka huu.
Mbali na majaribio hayo, bado mabasi yaendayo kasi yanakutana na changamoto zikiwemo za waendesha pikipiki, raia na daladala kupita kwenye njia ya mabasi hayo na kusababisha msongamano wa magari kitendo ambacho kinalazimu mabasi hayo nayo kujikuta yakikaa foleni.
Kupitia taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (Dart), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar es Salaam (Darcoboa), Sabri Mabrouk ni kwamba Daladala zote zinazofanya safari zake katikati ya jiji zimetakiwa kuondoka ifikapo Mei 2, mwaka huu huku akieleza kuwa tayari wamiliki wote wa mabasi walishalipwa fidia ya kubadili njia.
“Wamiliki wote wa mabasi wameshalipwa fedha zao tangu Desemba mwaka jana, hakuna anayedai na tumewapa siku saba kuondoka barabarani kabla ya Mei 2,” amesema Mabrouk.
(Picha na Salum Yasin / GPL)






