×

Jinsi ya kupika rosti ya nyama ya kusaga

nyama ya kusaga juu ya macaroni

Tayarisha sufuria safi, weka nyama ya kusaga peke yake bila ya kuweka maji. Changanya chumvi kiasi, tangawizi na kitunguu saumu.

Bandika mchanganyiko huo jikoni, ongeza maji kila mara pale nyama inapokaukia.

Funika ili nyama iive taratibu, hakikisha imeiva vyema. Baada ya kuiva epua nyama iweke kwenye chombo kingine pembeni.

Rudisha sufuria jikoni na weka mafuta ya kupikia kama vijiko vitatu, weka vitunguu maji endelea kukoroga mchanganyiko huo mpaka vitunguu  viive na kubadilika rangi, ongeza na pilipili moja nzima bila kuikata. Ongeza vipande vya viazi na karoti na koroga huku ukiongeza na bilinganya, pilipili hoho, nyanya, koroga kiasi kisha acha viive vizuri ili kutengeneza rojo.

Weka nyama ya kusaga korogahuo mchanganyiko kisha acha kidogo vikolee. Malizia na tui la nazi huku ukihakikisha unakoroga tui lisijekata. Baada ya tui kuiva vyema epua mboga yako tayari kwa kuchanganya na makaroni na kuliwa.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave a Comment