The House of Social Media
gunners X

Mimba kutunga nje ya mfuko wa kizazi- 2

0

Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke au Ectopic Pregnancy ni tatizo ambalo limetokea kuathiri wanawake mbalimbali. Kwa kawaida, isipokuwa mara chache sana, mimba zitungazo nje ya mfuko wa uzazi hazina uwezo wa kukua kuwa mtoto kamili.

Aidha, mimba hizi ni hatari kwa afya ya mama mjamzito kwa vile humfanya kupoteza damu nyingi na hatimaye kusababisha kifo. Baada ya utangulizi huo, wiki iliyopita tuliangalia aina za mimba zinazotungwa nje ya mfuko wa uzazi. Leo tutachambua aina hizo na sababu zake.

Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopio  (Fallopian Tubes).

Sababu kubwa inayosababisha mimba kutunga kwenye mirija ya Fallopian ni kushindwa kusafirishwa kwa kiinitete katika mirija hii hali inayotokana na mabadiliko katika hali ya mirija au uwezo duni wa mirija hiyo katika kusukuma kiinitete kuingia kwenye uterus kwa sababu ya ukosefu wa vinyweleo kutokana na magonjwa mbalimbali yanayoathiri muundo na maumbile ya mirija ya Fallopian.

Mimba zinazotunga kwenye mirija ya Fallopian huwa zina madhara makubwa zaidi kwa sababu eneo hili ni jembamba mno kuweza kuhimili ukuaji wa mimba na pia lina mishipa mingi ya damu inayopita karibu ambayo ipo hatarini kupasuka hivyo kusababisha mgonjwa kupoteza damu nyingi sana.

Mimba zinazotunga nje ya Uterus na nje ya mirija ya Fallopian

Baadhi ya mimba huweza kutunga kwenye kiwanda cha kuzalisha mayai (Ovary), kwenye shingo ya uzazi (Cervix) au ndani ya tumbo (Intra-abdominal).

Aina hii ya mimba ni chini ya asilimia tano ya mimba zote zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi.

Mimba inayotungwa ndani ya tumbo (Intra-abdominal) wakati fulani huweza kutoa mtoto aliye hai tofauti na aina nyingine za mimba zinazotunga nje ya uterus. Hata hivyo uzalishaji wake hufanywa kwa operesheni ingawa hakuna ushahidi wa kitabibu kuhusu suala hili mpaka sasa.

Madhara ya kutokea kwa upotezaji wa damu pamoja na maambukizi ni makubwa hivyo mara nyingi mimba za namna hii huhitaji kushughulikiwa haraka ili kumuepushia madhara makubwa mama mjamzito.

Mimba zinazotunga ndani na nje ya uterus kwa wakati mmoja.

Wakati fulani, mayai mawili yaliyorutubishwa kwa wakati mmoja hutokea kupandikizwa sehemu mbili tofauti. Moja likipandikizwa nje ya Uterus na jingine ndani ya Uterus. Katika aina hii ya Ectopic Pregnancy, uwezekano wa yai lililotungwa ndani ya Uterus kukua na kutoa mtoto ni mkubwa sana.

Mimba zinazojirudia kutunga nje ya mfuko wa uzazi

Wakati fulani hutokea kuwa, hata baada ya operesheni ya kuondoa mimba iliyotunga nje ya kizazi kufanyika, baada ya muda fulani seli za kiinitete huendelea kukua na kujitengeneza tena kufanya kusanyiko la seli kama mimba nyingine. Hali hii huitwa mimba zinazoendelea kutunga nje ya mfuko wa uzazi au Persistent Ectopic Pregnancy.

Kuna njia za kuepuka tatizo hili hivyo ni vema ukafuatilia makala haya wiki ijayo. Nikukumbushe kuwa, Sigwa Herbal Clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume, unaweza ukawatembelea katika vituo vyao vilivyopo nchi nzima kwa maelezo na msaada usisite kupiga simu zilizopo hapo juu.

Leave A Reply