×

‘Shika Ndinga’ na Efm Kinondoni usipime!

1.Washiriki wa shindano hilo wakishika ndinga .     Washiriki wa shindano hilo wakishika ndinga.

2.Washiriki wakiwa katika mapumziko baada ya raundi ya kwanza kumalizika. …Wakiwa katika mapumziko baada ya raundi ya kwanza kumalizika.

3.Mshiriki akikomaa na shindano hilo

Mshiriki akikomaa na pilkapilka za shindano hilo.

4.Baadhi ya mashabiki wa shindano hilo wakifuatilia kwa makini.

Baadhi ya mashabiki wa shindano hilo wakilifuatilia kwa makini.

5.

6.Baadhi ya pikipiki zilizotolewa kwa washindi (hawapo pichani).Baadhi ya pikipiki zilizotolewa kwa washindi (hawapo pichani).

7. Samwel Michael mkazi wa Kawe ndio mshindi kwa upande wakina baba.

 Samwel Michael mkazi wa Kawe ndiye mshindi kwa upande wa kina baba.

SHINDANO la Shika Ndinga  linaloratibiwa na kituo cha redio cha Efm  kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam, jana lilikuwa lilifana ‘kinouma’ baada ya  washindi kuibuka na pikipiki zao  katika viwanja vya Biafra Kinondoni, Dar.
Shindano hilo limeendelea  baada ya wiki iliyopita kufanyika katika Wilaya ya Ilala na  washindi wawili kupatikana  ambao ni Said Abdallah na Zainabu Mhagama ambapo wiki hii  limezikutanisha kata zote za Wilaya ya Kinondoni na kupatikana  washindi wawili ambao ni  Samweli Michael na Victoria Yobwa.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Meneja Mkuu wa Efm Redio, Dennis Ssebo, alisema  shindano hilo litaendelea  na washiriki 60 kwenye kila wilaya ambapo washiriki 10 kati yao,  wanawake watano na wanaume watano ambao wataingia katika fainali watajinyakulia gari aina ya Suzuki Carry.

Akifafanua,  Ssebo alisema  mwaka huu shindano hilo limeboreshwa zaidi kwa kutoa zawadi za pikipiki  kwenye ngazi ya wilaya na magari kwenye ngazi ya fainali, hivyo akaongeza kuwa washiriki hao walipatikana kutokana na kujibu maswali kwa ufasaha kupitia vipindi vya Efm Redio.

Alisema lengo la shindano hilo ni kuwawezesha wasikilizaji wa Efm  kwa namna moja au nyingine kuongeza na kukuza kipato kitakachochangia kuimarisha maisha yao kupitia zawadi watakazoibuka nazo.
Fainali za mwaka huu ambazo zitahitimishwa katika kiwanja cha TP kilichopo Sinza Dar.

Na Hilaly Daud/Gpl

Leave a Comment