Washiriki wa shindano hilo wakishika ndinga.
…Wakiwa katika mapumziko baada ya raundi ya kwanza kumalizika.
Mshiriki akikomaa na pilkapilka za shindano hilo.
Baadhi ya mashabiki wa shindano hilo wakilifuatilia kwa makini.
Baadhi ya pikipiki zilizotolewa kwa washindi (hawapo pichani).
Samwel Michael mkazi wa Kawe ndiye mshindi kwa upande wa kina baba.
SHINDANO la Shika Ndinga linaloratibiwa na kituo cha redio cha Efm kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam, jana lilikuwa lilifana ‘kinouma’ baada ya washindi kuibuka na pikipiki zao katika viwanja vya Biafra Kinondoni, Dar.
Shindano hilo limeendelea baada ya wiki iliyopita kufanyika katika Wilaya ya Ilala na washindi wawili kupatikana ambao ni Said Abdallah na Zainabu Mhagama ambapo wiki hii limezikutanisha kata zote za Wilaya ya Kinondoni na kupatikana washindi wawili ambao ni Samweli Michael na Victoria Yobwa.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Meneja Mkuu wa Efm Redio, Dennis Ssebo, alisema shindano hilo litaendelea na washiriki 60 kwenye kila wilaya ambapo washiriki 10 kati yao, wanawake watano na wanaume watano ambao wataingia katika fainali watajinyakulia gari aina ya Suzuki Carry.
Akifafanua, Ssebo alisema mwaka huu shindano hilo limeboreshwa zaidi kwa kutoa zawadi za pikipiki kwenye ngazi ya wilaya na magari kwenye ngazi ya fainali, hivyo akaongeza kuwa washiriki hao walipatikana kutokana na kujibu maswali kwa ufasaha kupitia vipindi vya Efm Redio.
Alisema lengo la shindano hilo ni kuwawezesha wasikilizaji wa Efm kwa namna moja au nyingine kuongeza na kukuza kipato kitakachochangia kuimarisha maisha yao kupitia zawadi watakazoibuka nazo.
Fainali za mwaka huu ambazo zitahitimishwa katika kiwanja cha TP kilichopo Sinza Dar.
Na Hilaly Daud/Gpl



