×

Lulu Diva aisikitikia afya ya mama yake

12912357_560722590775862_57615275_nLulu Abbas ‘Lulu Diva’

Stori: Imelda Mtema
Video Queen ambaye kwa sasa ni gumzo Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ameeleza jinsi anavyosikitishwa na afya ya mama yake mzazi ambaye ni mgonjwa anayelala kitandani muda wote.
Lulu aliitonya safu hii kwamba wanaomuona akicheka na kupiga mipicha akiwa anatabasamu wanahisi ana furaha sana lakini ukweli ni kwamba, kila akimfikiria mama yake furaha hutoweka.

“Niseme tu ukweli kwamba mama ndiyo kila kitu kwangu lakini hali yake kiafya inanikosesha furaha, yupo kitandani yapata mwaka sasa, wakati mwingine nalia weee, kisha namuachia Mungu, kinachomsumba naomba nisikiseme kwa sasa,” alisema Lulu.

Leave a Comment