
Msanii kunako anga la muziki wa Bingo Fleva Gift Stanford wengi wanamjua kwa jina la ’Gigy Money’ amesema kuwa Zuchu ni msanii ambaye amekuja kwa kasi na anajua anachokifanya kwenye muziki.
Akizungumza na Gazeti la Risasi Jumamosi Gigy amesema kuwa watu wafahamu kwamba vitu vizuri huwa havina papara, wala haraka ndiyo maana kila siku jina la Zuchu linazidi kukua, wasanii wanatakiwa kujipanga.
“Zuchu naweza kusema ni kiboko yao, ujio wa Zuchu ni mzuri, na anajua kuimba alafu watu wajue kwamba vitu vizuri havitaki haraka,wala havitaki papara na kwa haya anayoyafanya lazima Mungu amtendee miujiza’alisema Gigy.
Stori: Khadija Bakari