Noel Maruchilo akijaza kuponi yake ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.
Furaha Kalalu (kulia) akipewa maelekezo na Ofisa Masoko wa Global Publishers,Yohana Mkanda namna ya kujaza kuponi yake.
Msomaji wa Gazeti la Amani, Mussa Singo (kushoto) akijaza kuponi yake.
Mdau wa Gazeti la Amani aliyejitambulisha kwa jina moja la John, akishiriki kujaza kuponi yake.
Hussein Mwalami (katikati) akijaza kuponi yake.
Mmoja wa wasomaji wa Amani akishiriki kujaza kuponi yake.
Renard Steven naye akishiriki kujaza kuponi yake ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.
Joseph Alfred (kushoto) akipewa maelekezo na ofisa masoko wa Global namna ya kushiriki.
Fadhiri Mwambene naye akishiriki kujaza kuponi yake. Anayeshuhudia ni Ofisa Usambazaji wa Global, Jimmy Haroub.
ZIKIWA zimebaki siku 49 kabla ya msomaji mmoja wa magazeti ya Global Publishers kujishindia nyumba iliyopo Salasala jijini Dar, leo Alhamisi May 12, 2016 wasomaji wa Gazeti la Amani wa maeneo ya Kigamboni-Feri jijini Dar walionekana kuchangamkia Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba baada ya kulinunua gazeti hilo na kujaza kuponi.
Wasomaji walionekana kununua Gazeti la Amani na kujaza kuponi ili kuwezesha kushiriki droo ndogo na ya mwisho inayotarajiwa kuchezwa Mei 18, mwaka huu.
Naye Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda ambaye alikuwepo eneo hilo la Feri aliwaambia wasomaji kuwa;
“Siku zinazidi kuyoyoma na mshindi wa nyumba hiyo anaweza kuwa wewe, hivyo nunua magazeti ya Global mengi na kujaza kuponi ili kujiongezea nafasi ya kushinda.”
Droo kubwa inatarajiwa kufanyika mwezi ujao, ili kushiriki bahati nasibu hiyo, unachotakiwa ni kununua Magazeti Pendwa ya Uwazi, Amani, Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda na Championi.
Na Denis Mtima.Gpl









