×

Nani kuondoka na pikipiki wiki ijayo?

SHINDA NYUMBA (22)

Na Mwandishi Wetu

ZIKIWA zimebakia siku kadhaa kufikia Mei 18, ambapo droo ndogo ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa Magazeti Pendwa na Championi itafanyika, bado haijajulikana nani ataibuka mshindi wa pikipiki aina ya Skymark.

Akizungumza na Ijumaa, Afisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda alisema kuwa droo hiyo ambayo itakuwa ya nne tangu kuanza kwa droo ndogo itakuwa droo ya mwisho kabla ya kufanyika kwa droo kubwa ambapo mshindi atajinyakulia nyumba yenye samani zake iliyopo Salasala jijini Dar.

Alisema kuwa bado wasomaji wana nafasi za kujaza kuponi kwa wingi zinazopatikana katika magazeti hayo na kuzituma kwa wahusika.

“Wiki ijayo ndiyo utakuwa mwisho wa droo ndogo hivyo mshindi wa kwanza tutamzawadia pikipiki aina ya Skymark, mshindi wa pili simu ya kisasa ‘smartphone’, mshindi wa tatu, seti ya vyombo vya jikoni, mshindi wa nne mashuka na mwisho tutatoa ving’amuzi vitano kwa washindi watano,” alisema Mkanda na kuongeza;

“Napenda kuwasihi wasomaji wa magazeti yetu kutumia muda uliobaki kununua kwa wingi magazeti ya Global ili waweze kujaza kuponi na kuzikata kisha kuzileta ofisini kwetu, kwa mawakala wetu au      kwa njia ya Posta ili washiriki bahati nasibu kubwa ya nyumba ya kisasa.”

Katika droo ya tatu iliyofanyika Viwanja vya Manzese-Bakhresa, mwanamama kutoka Lushoto, Tanga, Zalika Ally alijishindia TV Flat Screen na king’amuzi chake.

Droo kubwa inatarajiwa kuchezeshwa mwezi ujao.

Leave a Comment