Abiria wakiwa katika dirisha la kukata tiketi eneo la kituo cha mabasi ya mwendo wa haraka Morocco-Kinondoni leo.
..Wakipita katika milango ya mashine za ‘kuskani’ tiketi baada ya safari yao kukamilika.
Abiria akipita baada ya kuskani tiketi yake kwenye milango maalum eneo la Morocco.
Abiria wengine wakiendelea kupita.
Basi la mwendo wa haraka likiingia katika kituo cha mabasi cha Morocco-Kinondoni jijini Dar.
ABIRIA leo wameanza kulipa nauli katika mabasi ya mwendo wa haraka (DART) yaliyoanza kufanya safari zake wiki iliyopita jijini Dar es Salaam baada ya siku zilizokuwa zimeongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, za kupanda bure kuisha.
Mtandao huu umefika katika kituo cha mabasi hayo kilichopo Morocco-Kinondoni jijini Dar na kukuta abiria wakikata tiketi huku wengine wakitoka katika safari zao licha ya baadhi ya abiria kuuambia mtaandao huu kuwa mashine za kukata tiketi zinakuwa hazifanyi kazi (kwa kupoteza netweki) ipasavyo na kusababisha foleni kwenye madirisha ya kukata tiketi.
Mwandishi wetu aliutafuta uongozi wa mradi huo wa mabasi (BRT) ili kuweza kuzungumzia kasoro hizo zilizotolewa na baadhi ya abiria lakini simu iliita bila kupokelewa.
NA DENIS MTIMA/GPL



