
Macho na masikio ya watanzania, wapenda muziki na dunia nzima siku ya Jumamosi na Jumapili Machi 12 na 13, 2022 yatakuwa jijini Dodoma kuserebuka kwa Tamasha la Muziki la Serengeti ambalo linaratibiwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini.

Tamasha hili limekuwa nyenzo adhimu ya umoja na mshikamanao kwa wasanii wote nchini lenye kuleta tija kwa tasnia ya muziki na taifa ambapo wasanii wanapata jukwaa la kuonesha talanta zao na kuburudisha jamii hata kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa.
Ikumbukwe, tamasha hili linafanyika kwa miaka wa mitatu mfululizo ambapo kwa mara ya kwanza lilifanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 2021 na mara ya pili ikafanyika jijini Dodoma Februari 2021 katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma
na 2022 linafanyika tena jijini Dodoma.