NSU ni herufi zinazotumiwa kuelezea magonjwa ya bakteria yanayoathiri mfereji wa kupitisha mkojo yaani Urethra kirefu chake ni Non Specific Urethritis.
Magonjwa hayo husambazwa kwa njia ya kufanya ngono isiyo salama.
Dalili:
Dalili zake hazionekani kwa urahisi kwa wanawake. Huenda zikaanza kwa kijidonda au kipele sehemu za siri za kike au za kiume au sehemu ya kupitishia haja kubwa. Kidonda hiki kinapopona usidhani ndiyo mwisho wa maambukizo la! Viini hivyo vinaweza kubaki mwilini kimyakimya kwa miaka mingi.
Lakini magonjwa mengine yanayoathiri njia ya mkojo kuanzia kwenye kibofu Bladder ni pamoja na kisonono, kwa mwanamke dalili huchelewa kujitokeza lakini baadaye atasikia maumivu makali sehemu ya tumbo.
Wanaume dalili huwa za haraka kwani hutokwa na usaha mbeleni na kuwashwa kwenye tundu la mkojo, kutokwa na ute na huenda akahisi maumivu wakati wa kukojoa. Kuna virusi vya kaswende ambavyo husababisha ugonjwa katika njia ya mkojo na husababishwa na bakteria waitwao Treponema Pallidum.
Matibabu:
Kabla ya tiba daktari atafanya uchunguzi wa damu kwani majimaji ya sehemu za siri huenda uchunguzi wake usioneshe viini vya kaswende. Kaswende ni hatari, kama haitibiwi, inaweza kusababisha utasa au ugumba na hata kuathiri moyo, mishipa ya damu, ngozi ya mwili, mifupa na hata ubongo na kurukwa na akili.
Hata hivyo, matibabu yake ni rahisi – Zipo dawa aina Antibiotics zinazoweza kutibu kaswende kabisa. Ili kuzuia kuenea kwa maradhi hayo ni vyema mpenzio naye pia atibiwe.
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP
*********
JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz