×

Ne-Yo atua Dar kwa kishindo, kufunika kesho Mwanza

NEYO DAR (1)

Staa wa Muziki wa R&B kutoka Marekani, Ne-Yo (katikati) akielekea kwenye gari baada ya kuwasili Dar.

NEYO DAR (2) NEYO DAR (3)

Warembo na wapenzi wa burudani wakimsubiri Ne-Yo.

NEYO DAR (4)

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom, Matina Nkurlu akiongea na wanahabari.

NEYO DAR (5)

Wanahabari na baadhi ya mashabiki wakati wakimsubiri staa wa Muziki wa R&B kutoka Marekani, Ne-Yo usiku wa kuamkia leo.

STAA wa Muziki wa R&B kutoka Marekani, Ne-Yo ametua usiku wa kuamkia leo ambapo anatarajiwa kupiga bonge la shoo kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Ne-Yo anayebamba na vibao vikali kama Because of You, Miss Independent na vingine vingi, alitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere mida ya saa tano akiwa ameambatana na timu nzima ya mabaunsa.

Akizungumza na wanahabari wakati alipowasili msanii huyo, Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania ambao ni miongoni mwa wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Matina Nkurlu alisema kuwa anafurahi kwa staa huyo kufika salama ndani ya nchi ya Tanzania sasa ni wapenzi tu wa burudani kukata tiketi kwa wingi ili waweze kushuhudia shoo hiyo.

“Ninafurahi Ne-Yo amefika salama na mashabiki wa burudani wakate tiketi kwa wingi kadri iwezekanavyo ili waweze kuja katika uwanja wa CCM kirumba Mwanza kesho na huduma mbalimbali kutoka Vodacom zitapatikana ndani ya uwanja huo,” alisema.

Shoo hiyo pia imedhaminiwa na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Global Publishers.

Leave a Comment