Makala: Boniphace Ngumije, RISASI JUMAMOSI
UKITIMBA katika ‘viunga’ vya Jiji la Nairobi ni rahisi sana kugundua kuwa hakuna msanii anayetengeneza ‘headlines’ kama Jackson Makini ‘Prezzo’. Huyu ni rapa ambaye mpaka sasa ana miaka 13 kwenye gemu la muziki nchini humo lakini bado hajakaukiwa mistari wala ‘interest’, watu wa burudani bado wanapenda kusikia lolote kutoka kwake.
Hata hivyo Prezzo ambaye ni Mkenya ‘mixer’ Mbongo, baba yake ni Mkikuyu na mama yake ni Mkurya aliyekulia Mwanza anasema katika ‘exclussive interview’ na Risasi Jumamosi kuwa sanaa ni sehemu ya maisha yake, yuko tayari kuwekeza pesa, nguvu na lolote lile ilimradi tu kulisukuma mbele gurudumu la sanaa.
KUHUSU KAZI
Prezzo ambaye hivi karibuni amemvisha pete ya uchumba Michelle Oyola anafunguka kuwa kazi zake za muziki anaziendesha mwenyewe, kwa sasa ana ‘project’ mpya ambayo iko mbioni kutoka aliyofanya na Hery Samir ‘Mr Blue’ lakini pia yuko Bongo kikazi, katika ‘tour’ iitwayo OnLine iliyoandaliwa na David Kallanja ‘Ervixy’, msanii kutoka lebo inayofanya vizuri Kenya kwa sasa Sappy Music.
“Pia tutashoot video ya Ervixy na reality show yangu iitwayo Nairobi Diaries ambayo inaendelea kuruka huko Kenya kila wiki. Vilevile niko katika mazungumzo na Barakah Da Prince akieleweka mimi na Ervixy tutafanya naye ngoma,” anasema Prezzo.
SKENDO
Skendo kwa prezzo ni sawa na chumvi kwenye mboga, yeye mwenyewe anadai kila kitu katika maisha yake ni skendo. Ambapo ukiachana na skendo ya kutoka na Loveness Malinzi ‘Diva’, Mtangazaji wa Kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Wema Sepetu kwa sasa staa huyu hana maelewano mazuri na mpenzi wake wa zamani mwanamuziki Huddah Monroe kufuatia kumvisha pete Michelle.
BIFU
Prezzo amewahi kuwa kwenye bifu na wasanii wengi akiwemo Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Kisa cha bifu lao, msikilize;
“Ishu yangu na Diamond ilitokana na mimi kutoka na Wema Sepetu alafu baadaye yeye alipokuwa naye akafahamu. Sasa wakati fulani, sikumbuki vizuri mwaka nilikuwa Bongo kuperfom kwenye Tamasha la Sabasaba, nilikuwa simfahamu kipindi hicho Diamond lakini kilichonishangaza nilimsikia katika mahojiano akiulizwa kuhusu mimi na kuniponda.
“Nilichukia kutokana na suala hilo ndiyo ukawa mwanzo wa bifu letu lakini hata hivyo bifu liliishia hewani,” anasema Prezzo.
Anaendelea kuwa amewahi pia kuwa kwenye bifu na msanii mwenzake wa Kenya, Jaquar lakini hiyo ilikuwa ni kiki ya mshikaji huyo ili kujulikana.
WAKENYA WANAMCHUKIA!
Prezzo anasema aliamini kuwa ndugu zake Wakenya hawampendi mwaka 2012 alipokwenda kwenye kinyang’anyiro cha Big Brother Africa. Sikia!
“Wakenya walipoona niko Big Brother waliongea sana, sijui ooh, huyu jamaa hana lolote anakwenda kutia aibu pia walikuwa hawanipigii kura kiasi kwamba kuanzia mwanzo mpaka natoka, kila wiki nilikuwa ninaingia kwenye danger zone.
“Hata hivyo always bad man (mara zote mtu mbaya) hakosi marafiki na maadui. Nakumbuka ndani ya Big Brother watu walipokuwa wakiulizwa nitoke walijitokeza wengi mpaka mstari unajaa, wakiulizwa niendelee pia wanajaza mstari,” anasema mkali huyo.
NI MUIGIZAJI PIA!
Mbali na kushika kimuziki Prezzo ni muuza nyago. Amefanya muvi iitwayo Cobra Squared pia ana mpango wa kufanya muvi nyingine lakini pia hivi karibuni anamalizia taratibu za kuandaa lebo itakayojulikana kwa jina la Makini Music Group. Mwisho ana malizia kuwa baada ya miaka miwili mbele hadhani kama ataendelea kufanya muziki ‘serious’.
KUHUSU ERVIXY NA SAPPY!
Hawa ni moja ya washikaji wanaoibeba Kenya kwa sasa kwenye tasnia ya muziki. Ervixy ambaye ni Mbongo kutoka Mwanza anayeishi Kenya amefanya ngoma iitwayo Basi na Belle 9 lakini pia kwa sasa yuko katika tour yake nchini iitwayo Online ambapo anapiga na wasanii wa Kibongo akiwemo Lina Sanga na anatarajia kufanya ngoma na Barakah Da Prince.
Kheri Kassim ‘Sappy’, yeye ni prodyuza ambaye jina lake limeanza kufahamika Bongo kupitia ngoma ya Joh Makini iitwayo XO. Sappy ndiye ‘official’ prodyuza wa Prezzo na Red San.
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP
*********
JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz


