STAA wa Ngoma ya Eminado kutoka Naija, Tiwa Savage amesaini rasmi lebo ya Roc Nation inayomilikiwa na staa wa Muziki wa Hip Hop, Shawn Carter ‘Jay Z’.
Kusaini kwa lebo hiyo inamaanisha bado Tiwa ataendelea kuitumikia lebo yake ya zamani ya Mavin Records iliyo chini ya Don Jazzy na wakati huohuo ataendelea kuwa chini ya mwavuli wa Roc Nation ambayo itakuwa ikimtengeneza kwenye ramani ya kimataifa zaidi hususan Marekani.
Hivi karibuni kupitia ukurasa wa Instagram wa Tiwa alitupia picha akiwa na Don Jazzy ndani ya Lebo ya Roc Nation, New York. Kusaini Roc Nation kunamfanya Tiwa kuwa staa wa muziki wa kwanza kutokea Nigeria. Mastaa wengine walio chini ya lebo hiyo ni Rihanna, Big Sean, DJ Khaled na wengine kibao.
