×

Yanga Wageuza Uchaguzi Kuwa Mkutano wa Kuchangia Ujenzi wa Uwanja

IMG_0491Wanachama wa Klabu ya Yanga wakitoa michango yao kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja.
IMG_0503Zoezi likiendeleaIMG_0508
Pesa zilizochangwa. IMG_0511(1)
Wanachama wa Klabu ya Yanga ghafla waliugeuza zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Klabu hiyo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kama harambee ya baada ya kuamua kuchanga fedha kwa ajili ya ujezi wa uwanja.
Ilikuwa ni baada ya msemaji wa klabu hiyo, Jerry Muro aliyekuwa akiongoza shughuli nzima kwenye uchaguzi kusema kuwa serikali ya awamu ya nne imewanyanyasa kwa kuwanyima kibali cha kuanza ujezi wa uwanja mbele ya DC wa Ilala, Raymond Mushi ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye zoezi hilo.
Kusema hivyo, wanachama walilipuka kwa kelele, kisha kuanza kumpelekea Murro stejini na kumuagiza amkabidhi DC ambaye pia alikuwa ameketi na Wajumbe Wakuu wa Bodi ya Udhamini, Mama Karume na Francis Kifukwe.

Haikujulikana mara moja kuwa ni kiasi gani cha fedha kilichochangwa leo kwa ajili ya kutimiza adhima hiyo ya kujenga uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo ya Yanga.

Leave a Comment