Moshi Katemi ‘Mo Music’ katika pozi tata na Tina.
BONIPHACE NGUMIJE
IMEVUJA! Mkali wa Ngoma ya Skendo, Moshi Katemi ‘Mo Music’ anadaiwa kutoka na demu wa msanii mwenzake wa Bongo Fleva, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ aliyefahamika kwa jina moja la Tina baada ya picha za mahaba za wawili hao kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa chanzo kilichomwaga ubuyu huo na picha, Mo amekuwa na ukaribu na mwanamke huyo kwa muda na wamekuwa wakionekana sambamba sehemu mbalimbali.
“Kwa sasa Mo haambiwi wala hasikii kwa huyo mdada ambaye anadaiwa kutoka pia na Nuh, wamekuwa
wakiambatana kama kumbikumbi,” kilisema chanzo.
Baada ya kunyaka ubuyu huo, Over Ze Weekend liliingia mzigoni na kumsaka Mo kujua ukweli ambapo alisema;
“Ni kweli nina ukaribu na huyo mwanamke lakini si wa kimapenzi na kuhusu Nuh sina uhakika juu ya hilo japo hivi karibuni niliona picha akimlisha keki Tina. Kingine ni yeye (Tina) aliyeomba kuwa karibu na mimi, nilikuwa simfahamu kabla kwa hiyo watu wasifikirie mambo mengine,” alisema Mo.
Alipoulizwa Nuh kuhusu ishu hiyo alisema Tina siyo mpenzi wake.
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP
*********
JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz
