×

Shilole alizwa na ‘akaunti yake’ ya matusi!

shilole (1)Stori: Hamida Hassan, Wikienda

DAR ES SALAAM: Staa wa muziki na sinema za Kibongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amelizwa na akaunti inayotumia jina la ‘Shilolekiuno_badgirlshishi’ kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram ambayo imekuwa ikitukana watu na kumsababishia ugomvi na wasanii wenzake.

Akizungumza na Wikienda, wikiendi iliyopita, Shilole au Shishi Baby alisema kuwa akaunti hiyo ambayo anadai kutengenezewa na watu wasiofahamika, imesababisha atukanwe na mashabiki wake kwani wapo wanaoamini ni yeye hivyo kujikuta akitumia muda mwingi kuwaelewesha kuwa hahusiani na akaunti hiyo.

“Kiukweli imenikosesha amani kwa sababu jina langu linatumika kutukana watu wa kila rika wakiwemo wasanii wenzangu hivyo nimeamua kuanza proces za kuhakikisha akaunti hiyo inafungwa na anayefanya hivyo akamatwe na mamlaka husika ya TCRA,” alisema Shilole.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave a Comment