×

V Money afurahia kolabo na Sauti Sol

V Money in Global TV Online (2)

STORI: BONIPHACE NGUMIJE

DIVA anayefanya poa kwa sasa kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Vannesa Mdee ‘V-Money’ hivi karibuni anategemewa kusikika kwenye kolabo mpya aliyopiga na wasanii kutoka Kenya wanaounda Kundi la Sauti Sol.

V-Money aliiambia safu hii kuwa, kolabo hiyo ambayo bado hajawa tayari kuvujisha jina lake ni ya pili kwake kufanya na wasanii wa nje kwa siku za hivi karibuni baada ya ile aliyofanya na 2Face Idebia kutoka Nigeria ambayo pia bado haijaachiwa rasmi.

“Nimefanya kolabo hivi mbili siku za karibuni na wasanii wa nje, nategemea zitaniongezea ujazo kwenye ‘fun base’ yangu kwa sababu wasanii ambao nimefanya nao kazi, wote wanafanya vizuri Afrika, pia wana mashabiki wengi,” alisema V- Money.

Leave a Comment