×

Pah One kumtumia Wema

Pah One, Ola, Igwe na TabanakoWasanii wanaounda Kundi la Pah One

STORI: BONIPHACE NGUMIJE

WASANII wanaounda Kundi la Pah One, Ola, Igwe na Tabanako wamefunguka kuwa wana mpango wa kumtumia diva mwenye ‘taito’ kubwa Bongo, Wema Sepetu katika shoo zao kutokana na mrembo huyo kuonesha moyo wa kuwaunga mkono na kupenda muziki wanaofanya.

wema_sepetu991Wema Sepetu

Akipiga stori ana kwa ana na safu hii Ola alisema kuwa wazo hilo la kumtumia Wema lilikuja baada ya juzikati kwenye tamasha la kuadhimisha miaka 10 kwenye game ya Christian Bella, mwanadada huyo kuonesha kupagawa na nyimbo zao wakati walipokuwa wanatoa burudani.

“Tumegundua Wema ni shabiki wa kazi zetu, tumekaa na kujadili na kuona ni vyema tufanye naye mazungumzo ya kibiashara ili awe anatupa kampani kwenye shoo zetu, mipango inafanyika na tunategemea haitakwenda kombo,” alisema Ola.

 

Leave a Comment