M SANII wa Bongo Fleva anayetamba kwa sasa na Wimbo wa Jike Shupa, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amesema kuwa kwa sasa amechoka kutegemea skendo za kijinga kumng’arisha badala yake atajitahidi kuboresha kazi zake akiamini hiyo ndiyo njia pekee ya mafanikio.
Nuh aliyasema hayo alipokuwa akipiga stori na gazeti hili ambapo alisema kama ni skendo amefanya sana lakini matokeo yake anaona maendeleo yake kimuziki yanajongea kwa mwendo wa kobe suala ambalo ‘sometimez’ linamkatisha tamaa.
“Sasa nataka nikomae tu kwenye kazi yangu ya muziki, kiki za kijinga hazina faida, watu wanataka muziki mzuri tu na ndicho nitakachofanya ili niwakune mashabiki wangu,” alisema Nuh.
