×

Raymond, Shetta na ushamba wao!

raymondRaymond wa WCB

STORI: MWANDISHI WETU

WASANII wa Bongo Fleva, Shetta na mwenzake Raymond wa WCB wamepondwa vikali kufuatia kuposti picha kwenye Mtandao wa Instagram wakiwa wamepiga na maburungutu ya fedha.

shettaShetta

Wadau wa muziki walioziona picha hizo walitoa maoni yao huku wengi wakiwaponda kuwa, huo ni ushamba kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa pesa hizo siyo zao.

“Hizi pesa watakuwa wameomba wapigie picha tu, haziwezi kuwa zao, halafu haya mambo ya kizamani kweli, yaani haina tofauti na kuazima gari ukapigie picha ili watu wajue unalo,” aliandika shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina Sosy P.

Hata hivyo, wapo waliosema huenda muziki umewalipa na pesa hizo ni zao ila wenyewe walipotafutwa ili kueleza kama ni zao au wameazima wapigie picha, hawakuweza kupatikana.

 

Leave a Comment