×

Ini Edo aachana na gym!

ini edo.jZIKIWA zimepita siku kadhaa Tangu tetesi kuenea kuwa Mkongwe wa fi lamu kutoka Naija, Ini Edo kanasa ujauzito, Habari ya mjini kwa sasa ni kuhusu Mwanadada huyo kuachana na Suala la kwenda gym.

Awali, Ini Edo anayedaiwa kuwa Na mimba ya miezi mitatu ya Mchumba wake ambaye ni msanii Mwenzake, Mike Godson alikuwa Akienda gym mara mbili kwa Siku lakini tangu anase kibendi Ameacha kabisa na mara nyingi Amekuwa ni mtu wa kujitenga.

Ini aliolewa Novemba 2008 Na mfanyabiashara aitwaye Philip Ehiagwina lakini walikuja Kuachana miaka mitano baadaye Ambapo Philip aliamua kuoa Mwanamke mwingine, Ruth. Ini Alibaki singo kabla ya mwaka jana Kumpata Mike.

Leave a Comment