×

Kidoa: Sijafungiwa ndani, nina ‘project’ zangu

KIDOA (3)Na Gladness Mallya

MWANADADA anayeuza sura kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Asha Salum ‘Kidoa’ amesema hajafungiwa ndani kama watu wanavyosema, isipokuwa ana ‘project’ zake za tamthiliya anayoicheza.

Kidoa alisema hayo kutokana na tetesi kuzagaa kwamba amekatazwa na ‘pedeshee’ wake asiendelee na kazi ya sanaa, kitu alichokanusha na kudai yupo bize na kucheza tamthiliya ambayo ameshirikishwa itakayotoka baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

“Hakuna mwanaume anayeweza kunizuia nisifanye kazi, labda akija yule mwenye malengo ya kutaka kunioa nitamsikiliza, lakini siyo hawa mapedeshee wa mjini ambao ni wa kupita tu, sijafungiwa ndani jamani ila niko bize tu na kazi ya tamthiliya,” alisema Kidoa.

Leave a Comment