MAPACHA wawili wamemuua mama yao mzazi na kuwajeruhi baba mzazi na kaka yao kwenye makazi yao yaliyopo Riyadh, Saudi Arabia baada ya kuzuiwa kujiunga na kundi lenye itikadi kali la wapiganaji wa ISIS.
Mapacha Khaled na Saleh al-Oraini wenye umri wa miaka 20, wamemwua mama yao Haila aliyekuwa na umri wa miaka 67, walikamatwa na kushikiliwa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo wakati wakijaribu kutoroka kwenye mpaka wa Yemen.
“Mbali na kumuua mama yao mzazi, pia walijaribu kumuua baba yao mzazi na kaka yao mkubwa ambao wamelazwa hospitalini kwa matibabu. 
Vilevile wanahusishwa na mauaji yaliyofanyika June 24 mwaka huu ambapo nchini humo watu kadhaa walijeruhiwa na kuuwawa”. Alisema Msemaji wa Jeshi la Saudi Arabia, Mansour al-Turki.



