Kisa Riyama… Mwana achaniwa nguo!
Riyama Ally
NA IMELDA MTEMA
DAR ES SALAAM: Msanii wa filamu anayekuja kwa kasi Bongo, Mwanaheri Ahmed hivi karibuni alikumbwa na dhahama alipokatiza Mtaa wa Kongo, Kariakoo jijini Dar baada ya kuchaniwa dera lake kisa kufananishwa na muigizaji mwenzake, Riyama Ally.
Mwanaheri Ahmed
Akizungumza na Amani Mwanaheri alisema kuwa, amekuwa akikutana na sintofahamu kubwa njiani baada ya watu wengi kumfananisha na Riyama hata kabla ya yeye kuingia kwenye uigizaji wa filamu.
“Aisee hivi majuzi watu walichana mkono wangu wa dera wakiwa wananivuta na kuniita Riyama huko
Kariakoo na hata siyo hivyo tu hata kabla sijaingia kwenye tasnia ya filamu wengi wananifananisha naye,” alisema Mwanaheri anayebamba na filamu yake ya Mwanaheri.