×

Gigy afanya kufuru nyingine ya za utupu!

Gigy-money-(4)

Stori: Hamida Hasssan, Wikienda

VIDEO queen anayefanya pia muziki na utangazaji Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amefanya kufuru nyingine baada ya kupiga picha ‘toleo jipya’ za nusu utupu ambazo zimezidisha uzito wa yale maneno kuwa mdada huyo hamnazo.

Gigy-money-(5)Picha hizo zipo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii zikimuonesha wazi sehemu kubwa ya mwili wake huku mwenyewe akionesha kutojali.

Gigy-money-(6)Baadhi ya picha hizo hata kwa dawa haziwezi kutimika kwenye gazeti kutokana na zilivyopitiliza kwenye ukiukaji wa maadili ya Kitanzania na alipopigiwa simu kuulizwa kulikoni alisema: “Jamani mimi ndivyo nilivyo, huo ndiyo mfumo wangu wa maisha kwa hiyo kama kuna mtu anakereka, ajinyonge kwa ‘bigijii’.”

Leave a Comment