KING wa R&B Bongo, Bernad Paul ‘Ben Pol’ anatarajiwa kuja na remix ya ngoma yake mpya ya Moyo Mashine akiwa amemshirikisha staa wa kimataifa (jina kapuni).
Akipiga stori mbili-tatu na mtandao wa Global Publishers, Ben Pol aliyewahi kubamba na Ngoma ya Sophia na Samboira alisema kuwa, mbali na remix hiyo pia atafanya ziara (Moyo Mashine Tour) nchi nzima.
“Ujue kwanza Moyo Mashine maana yake ni moyo kushindwa kuleta majibu ya upendo wakati kazi yake ni kuleta upendo. Nafurahi ngoma kupokelewa vizuri lakini niwaambie remix yake itakuwa mara mbili ya hii kwani nitatoka na staa wa kimataifa,” alisema Ben Pol.
