WAKATI gharama kubwa za video za Kibongo wanazofanyia nje ya nchi (Sauz na Nigeria) kufikia milioni 40, mamtoni ni kama kwenda disko na kipofu kwani video mpya ya staa wa Hip Hop Marekani, Kanye West ya Famous imegharimu dola milioni 750 (zaidi ya bilioni 1 za Kibongo).
Kwa mujibu wa Jarida la Life & Style, rapa Kanye West ametumia zaidi ya bilioni 1 kwa ajili ya kutengeneza sanamu zinazofanana na mastaa walioonekana kwenye video yake hiyo ambayo ni gumzo kwa sasa.
“Kanye ametumia zaidi ya miezi sita kusimamia matengenezo ya sanamu hizo na hata hivyo utayarishaji wa video ulichelewa kwa wiki sita kutokana na msanii huyo kutokuwa na furaha na muonekano wa mastaa hao,” ilisema sehemu ya jarida hilo.
Inaelezwa pia, katika video hiyo, Kanye hakutaka kutumia sanamu ya Caitlyn Jenner ambaye ni baba mkwe wake (aliyejibadilisha jinsia na kuwa mwanamke) na badala yake akatumia picha tu.
Video hiyo inawaonesha mastaa kibao ambao ni Kim Kardashian (mke wa Kanye), Ray J, Taylor Swift, Rihanna, Chris Brown, Donald Trump, Caitlyn Jenner, Bill Cosby, George W Bush na Amber Rose wakiwa kitandani nusu utupu.
