Tamari Ally ‘Tammy The Baddest’
ANDREW CARLOS
STAA wa Hip Hop Bongo anayebamba na Ngoma ya Trumpet, Tamari Ally ‘Tammy The Baddest’ kwa mara ya kwanza amekiri kuwa kipindi anataka kutoka kimuziki kuna kigogo wa serikali (jina linahifadhiwa) alitaka kumuoa kwa sharti la kuachana na muziki kwanza.
Akilonga na mtandao wa Global Publishers, Tammy anayejulikana pia kama Nicki Minaj wa Bongo alisema kutokana na kushindwa ‘kujimeneji’ kimuziki alimtafuta mtu wa kumuongoza ambapo aliangukia kwa kigogo huyo.
“Nashukuru Mungu kwa sasa nipo katika uhusiano na mpenzi wangu (Mnigeria). Nimepitia mapito magumu sana, kabla ya hapo kuna kigogo alikuwa akitaka niachane na muziki anioe nikamkatalia na kuachana naye kwani niliona anakatisha ndoto zangu,” alisema Tammy.