×

Ugonjwa wa mtindio wa akili (Mental Retardation)

Atr-xZipo sababu nyingi za mtu kupata tatizo la upungufu wa akili au mtindio wa akili Mental Retardation.

Kwa mtoto mdogo ni rahisi sana kujua kuwa ana tatizo hili kwani kuna dalili kama vile kuchelewa katika ukuaji wa uwezo wa kuongea/kuzungumza au anaweza kuwa na upungufu wa kumbukumbu au kuwa na matatizo ya kufahamu mambo ya kijamii.

Mtoto pia anaweza kuwa na tatizo la kuchelewa kukua kwa tabia za vitendo vya kujihudumia mwenyewe ama kuendelea kuwa na akili za kitoto na ikiwa anasoma basi atakuwa na upungufu katika uwezo wa kusoma na kushindwa kumudu masomo.

Mtoto mwenye dalili hizo anaweza kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam kama vile vipimo vya mfumo wa fahamu yaani mental status examination, vipimo vya mkojo kuangalia phenylketonuria, kipimo cha EEG kama amewahi kupata degedege, vipimo vya damu na kadhalika. Lakini pia mtoto anaweza kufanyiwa vipimo vya  saikolojia.

TIBA

Tiba ya mtu mwenye upungufu wa akili imegawanyika katika makundi mawili. Kwanza kwa kumpa mgonjwa huduma nyumbani na familia pamoja na familia kupewa elimu ya kijamii ili kuweza kumhudumia.

Pili mgonjwa apewe tiba sahihi kwa matatizo ya kisaikolojia na anayemuuguza aelimishwe kuhusu tabia za mtu mwenye upungufu wa akili. Mgonjwa anaweza kupewa dawa za ugonjwa wowote wa akili alionao antipsychotic medications.

USHAURI

Mtoto apelekwe katika shule maalum na mhusika apewe ushauri nasaha mara kwa mara au kuhudhuria programu maalum za ushauri nasaha na mambo ya kijamii.

Itaendelea wiki ijayo.

Dawa za maumivu kulingana na kiwango cha maumivu. Wagonjwa wa akili wasifanyiwe unyanyapaa na wafanyiwe uchunguzi mara kwa mara.

Zipo kinga ya awali (Primary prevention) kwa wagonjwa wa akili kama vile na kuboresha huduma za afya na kijamii ili kuondoa tatizo la utapia mlo, kuongeza uhamasishaji, kuondoa tatizo la kuzaa watoto njiti na kutoa elimu kwa kina mama wajawazito juu ya madhara ya madawa ya kulevya, unywaji pombe, magonjwa ya zinaa na n.k wakati wa ujauzito.

Ni vema pia kuboresha huduma za afya za kina mama, tiba ya magonjwa mbalimbali ili kuzuia maambukizi au madhara mbalimbali wakati wa ujauzito, kifafa cha mimba na magonjwa ambayo yanaweza kumuathiri mtoto kabla, wakati na baada ya kuzaliwa.

Ni vema pia kukumbuka kuwa mtoto apate chanjo dhidhi ya ugonjwa wa kifua kikuu, ugonjwa wa polio, ugonjwa wa surua na magonjwa yote yanayohitaji chanjo. Hii ni lazima kutilia mkazo kuwaelimisha kina mama wajawazito na wafahamishwe pia  madhara ya madawa ya kulevya na umuhimu wa kuhudhuria kliniki na ushauri nasaha utolewe kwa wazazi ambao wanaathari za viashiria vya asili (genetic counseling to high risk group).

Kinga ya baadaye yaani secondary prevention ni ya ugunduzi wa mapema na tiba sahihi kwa matatizo yanayoweza kuzuilika kama phenylketonuria au hypothyroidism  na pia kugundua mapema matatizo katika mfumo wa fahamu, mabadiliko ya tabia na hisia ili kukabiliana nayo mapema.

Ugunduzi wa magonjwa mbalimbali kama ugonjwa wa kaswende na magonjwa mengine ya zinaa kama kisonono mapema kwa wajawazito ni muhimu ili muathirika apate tiba haraka na mtoto asipate madhara.

Ni vema kufanya kipimo cha Ultrasound au CT na vingine ambavyo daktari ataona vinafaa ili kuweza kugundua kama mtoto ana kilema chochote katika maumbile, hii itasaidia kupanga na kumhudumia mapema zaidi ili kudhibiti tatizo.

Watu wengi walio na upungufu wa akili uliopitiliza (profound mental retardation) hufa katika umri mdogo au kabla ya kutimiza miaka 20.

Leave a Comment