×

Serikali Iangalie Upya Tamko Lake

Tanzania's President elect John Pombe Magufuli addresses members of the ruling Chama Cha Mapinduzi Party (CCM) at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam, October 30, 2015. Tanzania's ruling party candidate, John Magufuli, was declared winner on Thursday of a presidential election, after the national electoral body dismissed opposition complaints about the process and a demand for a recount. The election has been the most hotly contested race in the more than half a century of rule by the Chama Cha Mapinduzi Party, which fielded Magufuli, 56, a minister for public works. REUTERS/Sadi SaidNIMESEMA mara kadhaa na sioni tatizo kurudia. Ninamuunga mkono Rais Dk. John Pombe Magufuli ingawa sina imani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uongozi wa taifa letu. Imani kwa chama inapotea kwa sababu kwa nusu karne, kimeshindwa kusimamia vizuri rasilimali zetu kiasi kwamba maendeleo yetu hayafanani na tulichobarikiwa kuwa nacho na kinavyotumika.

Historia ya utendaji kazi wa Rais Magufuli ndiyo ulionifanya nimuamini na kumpigia kura ya ndiyo katika uchaguzi uliopita, licha ya ukweli kwamba kwa miaka mingi nimekuwa muumini mzuri wa upinzani. Na hata mwanzo mzuri wa uongozi wake, unanifanya kutojuta kwa nilichoamua, kwa sababu ameanza kwa kutembea mlemle ambamo Watanzania wamekuwa wakilia kwa muda mrefu.

Ufisadi, umungu mtu katika ofisi za umma, ufujaji wa fedha za serikali na kutowajibika kwa watumishi wa umma kimekuwa ni kilio cha siku nyingi cha wananchi, kwani matokeo yake nchi imedumaa kimaendeleo, huku maofisa wa serikali wakinufaika kwa utajiri wa harakaharaka pasipo mtu wa kuhoji juu ya utajiri wao.

Magufuli amekuja na kitu kinachoonekana kuwa dawa, kwani hata wale jamaa zangu wa bodaboda, ambao miezi nane nyuma walikuwa hawataki hata kulisikia jina hili, sasa ni mashabiki wake wakubwa na wanasema wazi kuwa hata upinzani, usingeweza kuucheza muziki huu.

Lakini katikati ya sifa na matarajio haya, serikali ya awamu ya tano imefanya makosa kadhaa, mojawapo ni hili la marufuku ya mikusanyiko ya kisiasa hadi mwaka 2020. Mwishoni mwa wiki iliyopita, bila shaka baada ya kuona harakati zinazofanywa na vijana wa upinzani mitandaoni, wakihamasishana kwenda kuuzuia mkutano wa CCM Dodoma, polisi wametoa tamko la nini kilichozuiwa.

Kwamba ni maandamano na mikutano ya hadhara, lakini ile ya ndani inayohusu utawala na utendaji ruksa. Hili ni tatizo. Kuzuia mikutano ya wanasiasa kwa kutoa sababu ya watu kufanya kazi, si utetezi wenye weledi. Mikutano ndiyo kazi ya wanasiasa, kuwazuia ni kutowataka wafanye kazi!

Lakini pia ni nani anamshurutisha mfanyakazi kwenda katika mkutano wa hadhara? Rais anapokwenda ziara za kikazi mikoani na kuzungumza na wananchi, ile siyo mikutano ya hadhara? Anafanya hivyo pia Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mawaziri na hata wakuu wa mikoa na wilaya.

Na wanapofanya hivi, wanazungumza siasa huku wakiwaponda wenzao wa upinzani. Kufanya hivi haki katika mchezo wa siasa. Wanasiasa watawasiliana vipi na wadau wao bila kukutana mikutanoni?

Siasa ni kazi namba moja katika maisha ya binadamu. Kila kinachotokea ni siasa, kama watu wanaonewa na polisi, wanadhulumiwa haki mahakamani, wanaporwa ardhi na viongozi, hawasikilizwi katika ofisi za umma, hawapati huduma stahiki na vitu vingine muhimu, watasemea wapi kama siyo katika mikutano ya mitaa yao, kata zao au vyama vyao?

Nachochea tu!

Leave a Comment