MKALI wa miondoko ya Afro Pop kutoka Nigeria, Peter Okoye ‘Mr Peter‘ aliyekuwa anaunda Kundi la P Square hivi karibuni ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instargram kuwa anakwenda kuwashitaki pacha wake Paul Okoye, kaka yao Jude na Mtandao mmoja wa simu wa nchini humo kwa kutumia picha yake katika matangazo ya tamasha la Paul lililofanyika siku chache zilizopita huko Goma, Kongo.
Mkali huyo aliyeamua kuachana na kundi na kubaki solo kufuatia tofauti za kifamilia, aliongeza kuwa si katika tamasha hilo tu ambalo jina lake linatumika kwenye picha ya pamoja akiwa na Paul, bali pia akwenye shoo inayokwenda kufanyika Agosti 17, mwaka huu huko Kinshasa, Kongo.