MKALI wa vichekesho Bongo, Musa Kitale ‘Kitale’ amefunguka kuwa tangu ajibatize jina la Mkude Simba na kuanza kukunja ‘chambichambi’ kupitia jina hilo kutokana na kufanya matangazo ya vichekesho amepata kiburi kiasi cha kukataa kufanya matangazo ya watu wengi ambao hawawezi kumlipa kiasi cha pesa ambacho anakuwa anakitaka.
Akipiga stori na mtandao wa Global Publishers, Kitale aliongeza kuwa kila mtu hufanya kazi kwa bidii ili thamani yake ipande na kuweza kupata mafanikio zaidi katika kile anachokifanya na si kunyonywa na wadau ambao wanafikiri wana nguvu katika kila kitu.
“Sifanyi kazi na mtu ambaye hafikii kiwango cha pesa ninachokihitaji mimi, siwezi kukiweka wazi lakini si haba na mtu anayetaka kufanya nami kazi lazima awe amejipanga,” alisema Kitale na kumalizia kuwa hiyo ndiyo sababu inayomfanya asionekane kwenye matangazo mengi.
