KAMPUNI ya Mawasiliano ya Huawei nchini kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni pamoja na Ofisi ya Polisi Mkoa wa Kinondoni, jana imetoa msaada wa vyakula nguo na vitu vingine kwa watoto yatima wa Kituo cha UMRA ha Magomeni-Mikumi jijini Dar.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria katika zoezi hilo ni Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Paulina Siara(kushoto), Maneja Mawasiliano na Mahusiano wa Huawei Tanzania, Jimmy Jin Liguo, Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Kinondoni, Veronica John na mwakilishi wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, Sadick Chuwa ambap waliishukuru kampuni hiyo kwa kuwajari wahitaji.
Aidha Mlezi wa Kituo wa kituo hicho cha UMRA, Riama Kishoma ametoa shukrani za dhati kwa kampuni ya Huawei kwa msaada waliotoa.