×

Kisa kuzimwa simu, njemba ala kichapo

KIBAKA (1) KIBAKA (2)NA RICHARD BUKOS, RISASI MCHANGANYIKO

DAR ES SALAAM: Njemba moja ambayo ilifahamika kwa jina la utani kama Mzee wa Ndole, mwishoni mwa wiki alikula kichapo chahaja, baada ya jaribio lake la kukwapua simu kushindikana, tukio lililotokea katika Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar.

KIBAKA (7)KIBAKA (4)Ikizungumzwa kuwa kuzimwa kwa simu feki kumesababisha bidhaa kuwa adimu kwa baadhi ya watu, Mzee wa Ndole alifikwa na masaibu hayo baada ya kumhadaa dada mmoja kuwa amepandwa na mdudu na hapohapo kujaribu kumwibia kifaa hicho cha mawasiliano.KIBAKA (3)

KIBAKA (8)Mashuhuda wa tukio hilo walisema Mzee wa Ndole alijifanya kumpangusa mdudu begani mdada aliyekuwa akipita njia na kumhadaa kisha kumchomolea simu yake aliyoichomeka kwenye sidiria.

KIBAKA (6)Mashuhuda hao walisema baada ya kipigo hicho, Mzee wa Ndole aliirudisha simu hiyo.

KIBAKA (5)

Leave a Comment