×

Thierry Henry aachia ngazi Arsenal

Thierry HenryzLONDON, England

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Arsenal Thierry Henry ameachana na klabu hiyo baada ya kocha mkuu Arsene Wenger kumwambia achague timu hiyo au kuwa mchambuzi wa soka wa Sky Sports.

Taarifa ya jana alifajiri ilitoka ikionyesha kuwa Wenger amemtaka kocha huyo wa vijana wa Arsenal kuchagua jambo moja, aidha kuwa mchambuzi wa Sky au kuwa kocha wa vijana wa Arsenal, majukumu ambayo alikuwa akiyafanya yote kwa wakati mmoja.

Thierry HenryWenger, 66, aliamini kuwa Mfaransa huyo hawezi kufanya majukumu yake ipasavyo kama atabaki hapo na wikiendi kwenda kuchambua soka kwenye televisheni.

Henry amekuwa akifanya kazi ya ukocha baada ya kufanikiwa kufuzu kozi ya ukocha hivi karibuni na amekuwa akitajwa mara kwa mara kuwa anaweza kuchukua nafasi ya Wenger akiondoka Arsenal.

Hata hivyo mchana wa jana ilitoka taarifa kuwa mshambuliaji huyo wa zamani aliamua kuachana na timu hiyo ambayo alikuwa akifanya kazi bure na kubaki Sky ambako analipwa pauni milioni 4, zaidi ya shilingi bilioni 9, kwa mwaka.

Mchezaji mwenzake wa zamani Tony Adams, amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi hiyo ya Henry kwenye timu hiyo.

Inaonekana kuwa Wenger na Henry hawakuwa kwenye uhusiano mzuri tangu mshambuliaji huyo wa zamani aliposema kuwa Arsenal haiwezi kutwaa ubingwa wa England kwa kumtegemea Olivier Giroud.

Leave a Comment