LONDON, England
KOCHA wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson amesema walimchagua kipa wa Ureno, Rui Patrício, kwenye kikosi cha wachezaji Bora wa Euro kwa kuwa alikuwa bora kwenye kila mchezo.
Ferguson alikuwa akisimamia paneli hiyo iliyokuwa inachambua kutafuta kikosi bora cha michuano hiyo, huku Ureno ikiwa ndiyo timu iliyoingiza wachezaji wengi kwenye kikosi hicho.
Ureno ambao ni mabingwa wa Euro walifanikiwa kuingiza wachezaji wanne ambao ni Patrício, Raphaël Guerreiro, Cristiano Ronaldo na Pepe.
Mbali na Ferguson kwenye paneli hiyo pia kulikuwa na Alain Giresse, David Moyes, Packie Bonner, Mixu Paatelainen, Savo Milošević, Peter Rudbæk, Gareth Southgate, Thomas Schaaf, Jean-François Domergue, Ginés Meléndez na Jean-Paul Brigger.
“Tulimchagua kila mmoja kwa ubora wake, tunaamini hii timu inaweza kufanya vizuri zaidi kwa kuwa kila mchezaji ameingia kwa vigezo vyake.
“Kipa wa Ureno tulimchagua hapa kwa kuwa alikuwa bora kwenye michezo yote ambayo timu yake ilicheza, hakika hiki ni kikosi bora zaidi,” alisema Ferguson.
Kikosi kamili ni kama ifuatavyo:
Mfumo (4-2-3-1):
Rui Patrício (Ureno); Joshua Kimmich (Ujerumani), Jérôme Boateng (Ujerumani), Pepe ( Ureno), Raphaël Guerreiro ( Ureno); Toni Kroos (Ujerumani), Joe Allen (Wales); Antoine Griezmann (Ufaransa), Aaron Ramsey (Wales), Dimitri Payet (Ufaransa); Cristiano Ronaldo (Ureno).

