MSANII wa Hip Hop Bongo, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ yupo kwenye mipango ya ‘kushuti’ video ya wimbo wake ambao unatambulika kama Pokopoko.
Dudubaya ambaye alikimbiza miaka ya nyuma kwa kutoa ngoma kali kama Dege la Jeshi, Nakupenda Tu, Mpenzi na nyinginezo kibao amesema kazi hiyo inakuja hivi karibuni.
Dudubaya au Mamba, ameiambia Mikito Jumatano kuwa, kichupa hicho cha Pokopoko ambao ni wimbo wake wa pili wa hivi karibuni baada ya Kokoriko utaanza kushutiwa hivi karibuni ambapo kwa sasa amedhamiria kupiga kazi kwa viwango vya juu.
“Video ya Pokopoko natarajia kuifanya hivi karibuni jijini hapa, lakini sasa ni mwendo wa kufanya kazi mara baada ya kumaliza mwezi wa Ramadhani ambao ulisimamisha baadhi ya vitu vyangu. Pia nina mpango wa kwenda kupiga shoo katika mikoa ambayo kwa kipindi kirefu sijafika kama Morogoro na Mbeya,” alisema Dudubaya.
