Askofu na Mwenyekiti wa Good News For All Ministry (Great Vision 2000) DK. Charles Gadi leo amezungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya kuliombea Taifa la Tanzania kwa siku 1001.
Maombi hayo yataanza rasmi Julai, 19 mwaka huu siku ya Jumanne katika Viwanja vya Biafra, Kinondoni jijini Dar sambamba na kuzunguka nchi nzima.
“Lengo la maombi hayo ni kuwahamasisha Watanzania katika ulipaji wa ushuru na kodi ili kukuza uchumi wa taifa letu, ulinzi wa miundo mbinu, wabunifu kwa kujiunga kwenye taasisi za vikoba, saccos na nyinginezo ili kuwa na kipato cha kuweza kuchangia kodi ya taifa.
“Kuhamasisha utalii wa ndani, kukagua afya mara kwa mara, kulinda maadili ya Kitanzania kwa watu wazima na wizazi vijavyo, suala la usafi, uzalendo wa kupenda na kununua bidhaa zinazozalishwa nchini na uboreshwaji wa huduma ya afya,” alisema DK.Gadi.
Na mwandishi wetu/GPL