×

Donald Trump na Vita ya Urais Marekani

10-donald-trump-debate.w750.h560.2x

Mgombea wa urais nchini Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump.

Na Leonard Msigwa/GPL

DONALD TRUMP ndiye mgombea wa urais nchini Marekani kupitia chama cha Republican akichuana na mgombea wa chama cha Democratic mwanamama Hillary Clinton. Je, nguvu ya Trump kuelekea uchaguzi mkuu wa Novemba 4 mwaka huu ikoje?  Je, nini hofu ya Wamarekani walio wengi juu ya nani hasa anafaa kuwaongoza?

 

Nguvu ya Trump ni kubwa  kwa sababu moja kubwa; raia wengi wa Marekani bado wana woga kwa nchi yao kuongozwa na mwanamke. Ikumbukwe kuwa tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1776 haijawahi kuongozwa na rais mwanamke, hivyo kutokana na historia hiyo Wamarekani wengi wanaogopa  kumkabidhi nchi Hillary Clinton.  Wanaona bora akabidhiwe Trump kwa kigezo cha mwanaume ambao wamekuwa wakitawala katika historia nzima  ya nchi hiyo tangu uhuru. Pia nchi hiyo ina changamoto nyingi  ambazo wana hofu mwanamke hataweza kupambana nazo.

CEDAR FALLS, IA - MAY 19: Democratic presidential hopeful and former Secretary of State Hillary Clinton hosts a small business forum with members of the business and lending communities at Bike Tech bicycle shop on May 19, 2015 in Cedar Falls, Iowa. Yesterday Clinton hosted an organizing rally with supporters in Mason City. (Photo by Scott Olson/Getty Images)

Mgombea wa chama cha Democratic mwana mama Hillary Clinton.

Hapo ndipo Trump anapopeta.  Endapo Democratic wangekuja na mgombea mwanaume mwenye ushawishi  na uzoefu wa uongozi basi uwezekano wa Trump kushindwa ulikuwa mkubwa. Kwa bahati mbaya chama hicho kimeshindwa kuja na mgombea wa aina hiyo, wote waliokuwepo wana uzoefu kidogo na mwanamama Hillary pekee ndiye mwenye sifa hizo, ila  tofauti yake ni jinsia tu.

 

Pamoja na Trump kupewa nafasi kubwa ya kushinda, wananchi wengi hawampendi kulingana na sababu zifuatazo.

 

Marekani ina tatizo kubwa la ubaguzi wa rangi kutoka kipindi cha utumwa hadi sasa, wengi wamepambana akiwemo Martin Luther King lakini tatizo hilo bado lipo. Wakati jamii bado inahangaika kulitatua tatizo hili, kitu cha ajabu Trump badala ya kuja na njia mbadala za kumaliza tatizo hili, anakuja na mpango wa kuwarudisha watu weusi Afrika. Ikumbukwe kwamba watu weusi nchini Marekani waliletwa tangu zama za utumwa kwa hiyo kutaka kuwarudisha Afrika ni kuwaonea maana wengi wao hawatakuwa na mahali pa kwenda.

 

Trump anaongelea suala la kutumia mabilioni ya dola kujenga ukuta wa kuweka mpaka halisi kati ya Marekani na Mexico, hivyo Wamarekani wengi wanahofia hili litaleta mgogoro mkubwa na linaweza kusababisha vita. Ikumbukwe kwamba Marekani ilipora jimbo la Texas kutoka Mexico.

 

Walichukua kinguvu wakati wa vita vya Hispania na Marekani mwaka 1898 wakati huo Mexico ikiwa koloni la Hispania. Vilevile, kwa sababu wakazi wengi  wa Texas ni wafanyabiashara wanaotegemea pia wateja kutoka nchini Mexico, wanahofia hatua hiyo itakwamisha biashara zao. Ikiwa ni pamoja na kwamba Jimbo la Texas ndiyo jimbo la kwanza kwa unafuu wa gharama za maisha, huenda hatua hiyo ikapandisha gharama za kila kitu, kitu ambacho wengi hawakubaliani nacho.

 

Katika sera zake, Trump amesisitiza kuhusu utengenezaji wa silaha za nyuklia. Amepanga kushirikiana na nchi ya Urusi na Korea Kusini kufanikisha mpango huo. Wengi wanaona hatua hiyo ni kuiweka dunia katika uwezekano wa kuzuka kwa vita ya tatu ya dunia, huku madhara yake yakidumu kwa muda mrefu kama yaliyotokea kwenye jimbo la Hiroshima na Nagasaki. Wengi wanahofia usalama wa mataifa madogo ambayo hawatengenezi silaha hizo lakini pia ni rahisi mataifa makubwa kuingia vitani.

 

Jambo jingine Wamarekani wanahofu kubwa kwamba Trump hana uzoefu wowote na masuala ya uongozi, tena uongozi wa juu kwenye taifa kubwa kama Marekani. Wengi wanamwona kama mfanyabiashara tu aliyebahatika kufanikiwa na amejaliwa kipaji cha kuongea. Wanaona ni sawa na kumkabidhi dereva mwanafunzi basi la abiria awafikishe wanakokwenda kwa sababu tu anaifahamu njia.

 

Pamoja na mabaya yote ya Trump, wananchi wengi bado wanaona nchi yao itakuwa mahali salama zaidi akikabidhiwa mwanaume kuliko mwanamke. Lakini pia bado ni mapema hatuwezi kutamka sasa kwamba Trump ndiye rais ajaye wa Marekani, kuna watu wengi bado wana imani na Hillary Clinton hasa wanawake.

 

Ikumbukwe wanawake wengi wa Marekani wana umoja wa kupigania haki zao, zamani walikuwa hawaruhusiwi kuajiriwa, kupiga kura ama kugombea nafasi za uongozi lakini waliungana na kupigania haki zao na leo wana uhuru sawa na wanaume katika masuala ya ajira na uongozi na sasa wanataka waongozwe na rais mwanamke.

 

Leave a Comment